KLABU
ya Everton imekubali kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu kiungo wa
Chelsea, Christian Atsu, kwa mujibu wa kocha Roberto Martinez.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ghana sasa anakwenda kupiga kazi Goodison Park kwa
msimu wote wa 2014/2015, kitu ambacho sasa Martinez amethibitisha.
Utaratibu
wa mkopo umefikiwa baina ya timu hizo mbili, huku kigali cha kufanya
kazi kikibaki kuwa kitu pekee kinachomchelewesha Atsu kuwa mchezaji wa
tano kusajiliwa na Everton msimu huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni