RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania bara, TFF,
Jamal Emil Malinzi amewashangaa watu wanaoshangilia shirikisho hilo kudaiwa
madeni na baadhi ya taasisi.
Kuna taarifa kuwa moja ya basi la timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars lipo katika hatari
ya kupigwa mnada na taasisi moja inayoidai TFF, ambayo Malinzi hakutaka
kuitaja, lakini wanajitahidi kutatua tatizo hilo.
Rais Malinzi amesema duniani kote hakuna taasisi
isiyodaiwa, hivyo si jambo la baadhi ya watu kusherekea.
“Hakuna taasisi isiyodaiwa madeni. TRA wenyewe
wanaokusanya kodi wana madeni, aibu kwa nani?, watu hawaelewi historia ya mpira
inavyokwenda,” alisema Malinzi.
“Kila siku nimezungumza, hata wakati wa siku 100
za kukaa madarakani nilisema madeni tunayodaiwa, tumejaribu kuyatatua. Mimi
siwezi kuja kwenye vyombo vya habari kusema madeni niliyorithi, huo sio
ustaarabu.”
“Lakini kama kuna mtu anashangilia eti TFF ina
madeni, huyu sio mwenzetu, lazima ajifikirie. Sio jambo la kusherekea”.
“Duniani kote hakuna chama wala Shirikisho
lisilokuwa na madeni, iwe Brazil, Ujerumani, Uingereza. Ni kiasi cha kila chama
kukata kipande cha nguo kinachotosheleza, mipango ya vyama ndio itatofautiana
kutokana na uwezo wa mapato.” Alisema Malinzi.
Malinzi aliongeza kuwa juzi juzi tu timu za Taifa zilicheza
mechi 4 za mashindano na TFF alizifanikisha ndani ya siku 14.
“Juzi tumecheza mechi nne kwa wiki mbili, vijana chini
ya miaka 17, na timu ya Taifa, Taifa Stars. Tumekuwa wenyeji nyumbani,
tumekwenda Afrika kusini, tumekwenda Msumbuji ndani ya siku 14. Hatuwezi kusema
tuna ukata, sema hatuna rasilimali za kutosha”. Alisema Malinzi.
“Hatuwezi kusema TFF imeshindwa hata hela ya maji, sema tunajitahidi kutafuta zaidi ili kujitoshekeleza kwa siku za usoni katika soka la wanaume na wanawake.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni