Wasiwasi: Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kuwa kuna timu hatari katika droo ya UEFA iliyofanyika leo ijumaa.
ASERNAL watakabiliana na Besiktas katika mchezo wa raundi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Arsene Wenger alikwepa kukutana na Athletic
Bilbao, Lille , FC Copenhagen, Standard Liege, lakini sasa atachuana na
timu hiyo ya Uturuki ambayo siku za karibuni ilimsajili Demba Ba kutoka
Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 4.7.
Besiktas ilimaliza katika nafasi ya tatu
msimu uliopita, lakini imefuzu kucheza UEFA baada mabingwa Fenerbahce
kufungiwa kucheza mechi za michuano ya ulaya kwa kosa la kupanga matokeo
ya mechi ya nyumbani.
Arsenal atacheza michuano ya ulaya kwa mwaka wa 17 mfululizo
Amefungiwa: Beki Bartosz Bereszynski alitolewa dakika za mwisho katika kipigo cha Celtic
Wachezaji wa Legia Warsaw wakishangilia baada ya dakika tisini, huku Stefan Johansen akiacha hoi.
Arsenal watasafiri kwenda Uturuki
kucheza mechi ya kwanza Agosti 19 au 20 mwaka huu na mechi ya marudiano
itapigwa Emirates Agosti 26 au 27.
Kiungo wa Asernal mwenye asili ya Uturuki, Mesut Ozil alifurahishwa na droo na kuandika kwenye mtandao wa Twita akisema: 'Droo nzuri! tayari tunaangalia mbele kuelekea mechi dhidi! @Besiktas! #Turkey #Ä°stanbul #Arsenal #AFC #UCLdraw'.
Wakati huo huo, leo asubuhi, Celtic wamepewa nafasi ya kusonga mbele baada ya kubainika kuwa klabu ya Legia Warsaw ilimchezesha mchezaji asiyekuwa na vigezo.
Kamati ya nidhamu ya UEFA ilikutana na
kutoa maamuzi kabla ya droo mjini Nyoni na kuamua kuwa Celtic wanatakiwa
kupewa ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa pili na inamaanisha
wamesonga mbele kwa magoli ya ugenini.
DRAW NZIMA HII HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni