Hussein Shariff, Manyika Peter Manyika, Mohammed
Hussein, Abdi Banda, Elius Maguli, Saad Kipanga....... watatambulishwa kesho katika
Tamasha la ‘ Simba Day’ katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tamasha hilo la kila mwaka ambalo hufanyika tarehe
8, Agosti ya kila mwaka lilianza kufanyika kwa mara kwanza msimu wa kiangazi
mwaka 2009 chini ya waasisi, Mzee Hassani Dalali na aliyekuwa katibu mkuu wa
klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwa lengo la kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya
za klabu huku pia lengo kiuchumi likiwemo .
Wachezaji hao wazawa wataungana na wachezaji wapya
wa kigeni, Paul Kiongera raia wa Kenya, Mrundi, Pierre Kwizera, na washambuliaj
raia wa Botswana, Jerome Ramathakwane na
Ousainou Manneh kutoka nchini Gambia katika mchezo maalumu dhidi ya Zesco ya
Zambia. Ambao watajaribiwa kwanza na kocha Zdravko Logarusic kabla ya
kusajiliwa.
Hussein Sharrif 'Casillas' naye atambaulishwa kesho
Tamasha hilo litafanyika kesho Agosti 9, kufuatia
siku ya leo kuwa na Tamasha la Matumaini na mashabiki wa Simba watapata fursa
ya kuona na kununua jezi mpya za klabu hiyo ambazo watazitumia msimu ujao.
Simba imejipanga kuhakikisha inaimarisha zaidi kikosi chake ndiyo maana
wamekuwa ‘ busy’ kusaka wachezaji wakati huu dirisha la usajili likikaribia
kufungwa.
WACHEZAJI SABA WA KIGENI
Donald Musoti, Amis Tambwe, Joseph Owino,
Kiongera, Kwizera, Jerome, na Manneh watakuwepo uwanjani siku ya kesho.
Wachezaji hao wote ni raia wa kigeni na wamekuja kwa ajili ya kuifufua Simba
baada ya kuwa na misimu miwili mibaya katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Simba
inaweza kuwasaini wachezaji wote hao kama mwalimu Logarusic ataridhika na
viwango vyao kwa sababu sheria ya wachezaji wa kulipwa itabadilishwa na kufikia
wachezaji saba.
Abdi Banda atatambulishwa kesho 'Simba Day'
Hii ni mara ya kwanza kwa Tamasha la Simba Day
kuwa na wachezaji saba wa kigeni na ni wakati mwafaka kwa mashabiki wa klabu
hiyo kujitokeza uwanjani siku ya kesho kwa lengo la kwenda kuitazama timu yao
mpya ambayo inasukwa katika mtindo wa kimataifa.
Ligi kuu inataraji kuanza kutimua vumbi lake,
Septemba 20, hivyo baada ya Tamasha hilo timu itakuwa na muda mrefu wa
kujiandaa na kutengeneza timu kabambe ambayo itaweza kutoa ushindani kwa timu
za Yanga SC, Azam SC, Mbeya City ambazo zimeoneka kufanya usajili makini zaidi
licha ya kumaliza katika nafasi tatu za juu msimu uliopita.
Wachezaji kama nahodha Nasorro Masoud ‘ Collo’,
Amri Kiemba, Issa Rashid, William Lucian, Jonas Mkude, Said Ndemla, Miraji
Adam, Abdallah Seseme, Ibrahimu Twaha, Ramadhani Singano, Haroun Chanongo,
Uhuru Suleimani, Ivo Mapunda wataungana na wachezaji wapya waliosajiliwa
klabuni hapo siku ya kesho huku mwanamuziki nyota nchini, Diamond Platnumz
akitaraji kutumbuiza kabla ya zoezi la utambulisho wa wachezaji kuanza. Itakuwa
siku ya aina yake kwa wapenzi wa klabu hiyo.
NI SIKU NZURI KWA KUSAIDIA UJENZI WA UWANJA WA
KLABU
Wiki iliyopita Simba ilianza kufanya mazoezi
katika uwanja wake wa wazi huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na
juzi wanachama wa tawi la ‘ Home Boys Wazo Hill’ waliahidi kutoa tani 10 za
mifuko ya saruji ili kusaidia uendelezaji wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo
ambao unaendelea. Simba inaweza kutumia Tamasha hilo kuwaunganisha wanachama
wake ambao walikuwa katika tofauti miaka ya karibuni kutokana na uongozi mbaya
wa utawala uliopita. Kila mwanachama wa Simba anaweza kujitolea kwa namna
anavyoweza kwa sababu wanachama ndiyo sehemu muhimu ya kuijenga klabu hivyo ushirikiano ni muhimu kuanzia kwa
viongozi, wanachama, wachezaji na benchi la ufundi. Simba Day ina maana kubwa
na wanachama wanaweza kutumia nafasi yao kusaidia kwa hali na mali klabu yao.
Kila la heri Tamasha la Simba Day…..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni