Tuzo: James Rodriguez amekuwa mchezaji wa kwanza wa Colombia kushinda kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao sita.
NYOTA mpya wa Real Madrid, James
Rodriguez amesema kushinda kiatu cha dhahabu katika fainali za kombe la
dunia ilikuwa ndoto iliyotimia.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23
aliposti picha katika mtandao wa Twita akiwa na tuzo ya kiatu cha
dhahabu aliyoshinda baada ya kufunga mabao sita katika fainali za kombe
la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Ili kushangilia tuzo hiyo, nyota huyo wa
Colombia atacheza msimu ujao kwa kutumia viatu vya dhahabu na
anatarajia kuongeza mabao mengi zaidi.
"Nilikuwa na
matumaini ya kushinda kwasababu mara zote nilikuwa naota kushinda kitu
kama hiki,' James aliwaambia waandishi. 'Hii pia ni chanzo cha furaha
kwa nchi yangu ya Colombia. Kwasababu walinipa nguvu sana, kwahiyo
nilitakiwa kushinda tuzo.'
Viatu vipya: Kiungo huyu wa Colombia atachezea viatu vya dhahabu msimu ujao kama sehemu ya kusherehekea mafanikio.
MABAO YA RODRIGUEZ KOMBE LA DUNIA 2014
- Alifunga moja, na kutengeneza moja dhidi ya Ugiriki.
- Alifunga moja, na kutengeneza moja dhidi ya Cameroon
- Alifunga bao zuri dhidi ya Japan
- Alifunga mabao mawili dhidi ya Uruguay, likiwemo bao la mashindano
- Alifunga penati Colombia wakifungwa 2-1 na Brazil katika mchezo wa robo fainali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni