Manchester United
wanajiandaa kuwekeza kitita cha kutosha ili kuinasa saini ya Angel Di
Maria kutoka Real Madrid.
MASHETANI wekundu, Manchester United
wanajiandaa kumwaga paundi milioni 100 kumshawishi Angel di Maria kutua
Old Trafford wakati huu klabu inahitaji kujiboresha ili kushindania
ubingwa wa ligi kuu England.
Kocha mkuu wa United, Louis Van Gaal
anahitaji kusajili wachezaji wa kiwango cha dunia kabla ya kufungwa kwa
dirisha la usajili barani ulaya na tayari ameshaonja machungu ya
kufungwa ambapo alilala mabao 2-1 dhidi ya Swansea jumamosi iliyopita
uwanjani Old Trafford.
Mkurugenzi mkuu wa United, Ed Woodward
amemuunga mkono Van Gaal na yupo tayari kufanya lolote lile ili mradi Di
Maria atue Man United.
Inafahamika kuwa United imemuambia
Muargentina huyo kwamba kwa kiwango chake cha sasa itamlipa mshahara wa
paundi laki mbili kwa wiki.
Kwa mkataba wa miaka mitano anaotarajiwa
kupewa, United itawezekeza paundi milioni 100 ikijumuisha mshahara wake
na ada ya uhamisho.
Di Maria anajua kuwa Man United wapo tayari kumlipa mkwanja mrefu ili atue Old Trafford.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni