Ugonjwa wa Ebola unaendelea kuwa tishio kubwa kwa watu Afrika Magharibi huku idadi kubwa ya watu ikipoteza maisha.
Kufuatia hofu
ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari kwa kugusa au kuwa karibu na wagonjwa
au miili ya waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo, ndugu wa marehemu
wameripotiwa kuiburuza miili ya ndugu zao kutoka majumbani kwao na
kuitupa hovyo mitaani hali inayoongeza hatari zaidi ya maambukizi.
Kwa mujibu wa Daily Mail, ugojwa huo hatari unaoweza kusababisha mtu
kutokwa na damu machoni, mdomoni na masikioni umeshaua takribani watu
9,000 katika nchi za Afrika Mashariki.
Madaktari wanaohudumia wagonjwa wa Ebola wanapata changamoto kubwa ya
kukwepa maambukizi huku baadhi yao wakiripotiwa kupata maambukizi na
kupoteza maisha.
Hali ya hatari imesababisha abiria wanaosafiri kutoka Afrika Magharibi
kufanyiwa vipimo katika viwanja vya ndege kwa hofu ya kuusambaza ugonjwa
huo katika nchi wanazokwenda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni