Kipa wa Simba, Hussen Sharrif 'Casillas'
KOCHA wa Makipa wa
Simba, Iddi Pazi, amesema kitendo cha kocha mkuu wa timu hiyo, Zdravko
Logarusic kuonyesha kutokumkubali kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ aliyesajiliwa
kikosini hapo kutokana na kuwa na mwili mdogo, kimepandisha morali ya kipa huyo
na ameapa kumshawishi kocha huyo kwa njia zote ili ampatie nafasi kikosini
hapo.
Logarusic alipendekeza
klabu hiyo isajili kipa mwenye uwezo wa juu na mwenye mwili mkubwa, lakini
Kamati ya Usajili ya klabu hiyo iliposhindwa kumpata kipa mwenye vigezo hivyo
viwili, iliamua kumsajili Casillas ambaye ndiye alikuwa kipa bora msimu uliopita
alipoichezea Mtibwa Sugar.
“Bado naendelea na
programu yangu ya kumpatia mazoezi makali, maneno ya kocha yalionekana
kumkatisha tamaa mwanzoni, lakini kwa sasa morali yake iko juu, ameapa
kumwonyesha kocha Logarusic kuwa umbo si kitu,” alisema Pazi.
“Kwa siku chache
nilizomfanyisha programu yangu hiyo, ameonekana kuipenda, ameanza kunipa moyo
kuwa kwa siku zijazo ataweza kumshawishi kocha akasahau kabisa kuhusu udogo wa
umbo lake.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni