 
Mwaka mgumu: Phil Neville alisema msimu uliopita ulikuwa wa majanga kwa Manchester United chini ya David Moyes.
PHIL Neville amekiri kuwa kumteua David Moyes kuifundisha Manchester United lilikuwa janga kubwa.
Neville, ambaye aliteuliwa na Moyes kuwa
 kocha msaidizi namba moja msimu uliopita alisema: 'Wote tulitakiwa 
kuwajibika, sio David Moyes tu. Niliwajibika na wengine waliohusika 
walitakiwa.
'Mwaka uliopita ulikuwa ni janga kwelikweli, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.'
 
Muda wa majanga: Moyes alimaliza katika nafasi ya 7 licha ya kupewa klabu ikiwa ni bingwa mtetezi.
Lakini Neville anaamini, United inaweza 
kurudi vizuri kutoka kwenye nafasi mbaya zaidi waliyomaliza ikiwa 
imepita miaka 24: 'Nadhani tunaenda kushinda kombe,' alisema. 'Nafasi ya
 pili sio nzuri kabisa kwa Manchester United.
'Tumepata nafasi nzuri mwaka huu kwasababu hatuna michuano ya Ulaya.
'Ni kuwaunganisha pamoja na wachezaji 
wote wanaonekana kuwa tayari kushinda ligi tena baada ya kutoka kwenye 
maandalizi ya msimu'.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni