KIKOSI cha pili cha Azam fc
kimepigwa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi maalumu ya kirafiki ya
Tamasha la Usiku wa Matumaini usiku wa jana kwenye
uwanja wa Taifa, uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
uwanja wa Taifa, uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
Kwa ushindi huo, wakata miwa wa
mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro wamefanikiwa kutwaa Ngao ya
Matumaini.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa
maalumu kwa kocha mkuu wa Mtibwa, Mecky Mexime kuonesha wachezaji wake jinsi
walivyoiva, wachezaji wawili wakongwe, Musa Hassan Mgosi na Vicent Barnabas
walionesha kandanda la kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
Baada ya mechi ya leo , kikosi hicho cha Azam kitasafiri muda wowote kuelekea mjini Kigali nchini Rwanda kikifuata kikosi cha kwanza kinachoshiriki kombe la Kagame.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni