Majembe ya kazi: Manahodha
wa Barcelona kutoka kushoto Sergio Busquets, Lionel Messi, Xavi na Andres
Iniesta
KIUNGO mkongwe, Xavi Hernandez ameteuliwa kuwa
Nahodha mpya wa wazee wa Katalunya, FC Barcelona kuanzia msimu ujao.
Kitambaa cha unahodha wa Barca kimeachwa wazi na
beki Carles Puyol aliyestaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita na kura
zikapigwa kumpata atakayerithi mikoba yake.
Nyota huyo wa Hispania, alishinda kura zilizopigwa na kutangazwa rasmi jana kuwa Nahodha Mkuu, akifuatiwa na Andres Iniesta, Lionel Messi na Sergio Busquets, ambao watakuwa Manahodha Wasaidizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni