SIMBA
SC imevunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic siku moja
tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika
mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
.
Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kwamba Logarusic amevunjiwa Mkataba kwa kukiuka masharti ya mwajiri wake na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakuwa kaimu kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

Loga
ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa
amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu na kikubwa ni kuwatolea maneno
yasiyofaa wachezaji.
Inaelezwa Loga alifikia hatua ya kuwadharau na kuwatolea maneno yasiyofaa hadi viongozi wa klabu hiyo.
Loga
anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba
mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga
aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Patrick Liewig aliikuta Simba SC bado
ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza
nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni