TIMU
ya magwiji ya Manchester United imetoa safe ya kufungana mabao 3-3 na
magwiji wenzao wa Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena.
Mshambuliaji Andrew Cole aling'ara katika mchezo huo akifunga mabao mawili akicheza pamoja na pacha wake wa zamani, Dwight Yorke wakichezeshwa na kiungo Paul Scholes.
Lee Martin alimtilia Cole krosi ya chini kufunga bao la kwanza dakika ya tisa akimtungua Hans-Joerg Butt langoni mwa Bayern.
Paulo
Sergio akafunga bao la kusawazisha dakika mbili baadaye, akimtesa
Tomasz Kuszczak baada ya kumpeleka kipa huyo wa Poland sehemu tofuti na
mpira.
Mshambuliaji wa zamani wa Brazil, Giovane Elber akaifungia bao la pili Bayern kabla ya Scholes kumsetia Yorke kuisawazishia United. Alexander Zickler akaifungia tena bao la ushindi Bayern kabla ya Cole kuwafungia Mashetani Wekundu bao la kusawazisha zikiwa zimebaki dakika saba.
Kikosi
cha Manchester United kilikuwa: Kuszczak, Irwin, Johnsen, Dublin,
Martin, Blomqvist, P. Neville, Scholes, Fortune, Cole na Yorke.
Bayern Munich: Butt, Babbel, Kreuzer, Kovac, Pflugler, Van Bommel, Thon, Sergio, Breitner, Zickler na Elber.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni