Mlinda lango: Kipa mwenye urefu wa futi 6 na inchi saba amekamilisha usajili wake kuhamia Southampton kutoka Celtic
KLABU
ya Southampton imekamilisha usajili wa kipa wa England, Fraser Forster
kwa dau la Pauni Milioni 10 kitoka mabingwa wa Scotland, Celtic.
Kocha
wa Watakatifu, Ronald Koeman amesema jana baada ya kipigo cha 1-0
katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu kutoka kwa Bayer Leverkusen
kwamba dili ni kama limetimia baada ya klabu hizo kukubaliana ada ya
uhamisho na mchezaji tayari amefanyiwa vipimo.
Na
Jumamosi jioni klabu hiyo ilitoa taarifa kwenhye tovuti yake
ikithibitisha usajili wa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 26.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni