Shujaa wa leo: Fellaini (wa tatu kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi
KOCHA
Louis van Gaal ameendelea kuwapa raja mashabiki wa Old Trafford baada
ya Manchester United jana kuifunga Valencia mabao 2-1 katika mchezo wa
kirafiki.
Sifa zimuendee Marouane Fellaini aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao, Wayne Rooney alikosa penalti kipindi cha kwanza iliyookolewa na Diego Alves.
United ilitangulia kupata bao kupitia kwa Darren Fletcher dakika ya 49 kabla ya Rodrigo kuisawazishia Valencia dakika ya 71.
Kikosi cha Manchester United: De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Young, Fletcher, Herrera, James; Mata; Rooney, Hernandez
Valencia: Alves; Barragan, Vezo, Otamendi, Gaya; Parejo, J. Fuego, Andre Gomes; Feghouli, Alcacer, Rodrigo
Marouane Fellaini akiifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Valencia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni