KLABU
ya Aston Villa imetangaza kumsajili beki wa Ufaransa, Aly Cissokho
kutoka Valencia, na sasa linashughulikia suala la uhamisho wa kimataifa.
Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 amekubali mkataba wa miaka minne kuingia kikosi cha Paul Lambert.
Villa
imetangaza kwenye akaunti yake ya Twitter, ikisema: "Aly Cissokho
amejiunga nasi kwa mkataba wa miaka minne @ValenciaCF, kinachofuata ni
uhamisho wa kimataifa,".
Uhamisho:
Valencia ilimsajili Cissokho kutoka Lyon kwa Pauni Milioni 5 miaka
miwili iliyopita, lakini sasa inaweza kumuuza kwa bei nusu ya hiyo
Cissokho
anaungana na wakali kama Kieran Richardson, Joe Cole na Philippe
Senderos katika orodha ya wachezaji wapya Villa Park na usajili wake
unaweza kugharimu Pauni Milioni 2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni