MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wamelazimisha suluhu tasa ya bila kufungana na wenyeji Rayon Sport katika mchezo wa pili wa kundi A kombe la Kagame lililoanza kutimua vumbi jana viwanja viwili tafouti nchini Rwanda.
Katika mechi nyingine, KMKM imetoka sare ya kufungana
bao 1-1 dhidi ya Atlabara ya Sudan kusini katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa
mapema katika uwanja wa Amahoro.
Wawakilishi hao wa Zanzibar walikuwa wa kwanza kupata
bao la kuongoza katika dakika ya 29 kupitia kwa Mudrik Abdullah akiunganisha
kwa kichwa krosi ya Moka Msafiri, lakini beki Makame Mngwali wa KMKM alijifunga
katika jitihada za kuokoa dakika chache baadaye.
Mchezo mwingine uliopigwa leo umewakutanisha KCC
ya Uganda dhidi ya Gor Mahia ya Kenya na kushudia wawakilishi hao wa Uganda
wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kesho Agosti 9 mwaka huu katika dimba la
Amahoro mechi mbili za kundi C na moja ya kundi B zitapigwa.
Mapema itaanza mechi ya mabingwa Vital’O ya
Burundi dhidi ya Benadir ya Somalia ikifuatiwa na mechi ya jioni baina ya
Police ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan.
Baadaye usiku maafande wa jeshi, APR ya Rwanda
watachuana na Flambeau ya Burundi.
Azam fc watashuka dimbani tena Agosti 10 mchana kuchuana na KMKM ya Zanzibar, mchezo wa kundi A.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni