Wakati
Real Madrid wameibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Elche, Barcelona
mambo yamekuwa si safi kiivyo baada ya kulazimishwa sare ya suluhu
dhidi ya Malaga.
Wakiwa
ugenini, Barcelona walifanya kila juhudi huku mshambuliaji wao nyota
Lionel Messi akihaha kila idara ili kupata bao angalau moja, lakini
mambo yalishindikana.
Wakati
fulani, Malaga walikuwa wakali kama nyuki katika mechi hiyo ya La Liga
lakini kipa wa Barcelona akawa imara kuokoa michomo ya hatari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni