Louis van Gaal na Ryan Giggs walioneka kushitushwa na kipigo dhidi ya Leicester
IMETAARIFIWA kuwa Louis van Gaal
aliwacharukia wachezaji wa Manchester United kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo kufuatia kipigo cha 5-3 kutoka kwa Leicester.
Van Gaal aligeuka mbogo akiwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza uongozi wa 3-1 na kumaliza mechi kwa kipigo kizito.
Kocha huyo mwenye heshima ya kutokuwa na
hasira na wachezaji wake, aliwakalipia waziwazi baada ya kufungwa kwa
mara ya pili katika michuano ya ligi kuu England.
Wachezaji wa Manchester United United wakionekena wamekata tamaa baada ya kufungwa goli la tano katika uwanja wa King Power
Wachezaji wa United wakishangilia bao la Ander Herrera lililowafanya wawe mbele kwa mabao 3-1
United walipata kipigo cha aibu na kumuacha Van Gaal na hasira za ajabu.
Van Gaal alikuwa na Radamel Falcao,
Wayne Rooney na Van Persie katika kikosi kilichoanza, lakini baadaye
alilalamika akisema: "Tuna wachezaji wengi ambao hawatafuti magoli."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni