Mario Balotelli alipokea ujumbe wa
kibaguzi katika twita hiyo hapo juu kutoka kwa mashabiki wa Manchester
United baada ya kufungwa 5-3 na Leicester City jana.
POLISI wameanza kufanya uchunguzi juu ya
tuhuma za ubaguzi wa rangi aliofanyiwa mshambuliaji wa Liverpool, Mario
Balotelli katika mtandao wa kijamii wa Twita.
Taarifa kutoka kituo cha polisi cha Merseyside
imesomeka: "Tunaweza kuthibitisha kuwa maofisa wanachunguza maoni ya
kibaguzi yaliyotolewa kwa Balotelli katika mtandao wa Twita ".
Balotelli alishitushwa na kipigo
walichopata United, muda mfupi baada ya timu yake ya Liverpool
kutandikwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham siku ya jumamosi na alitweet: : 'Man Utd...LOL' akijibu kipigo cha mabao 5-3 katika uwanja wa King Power Stadium.
Twita yake ilikumbana na ujumbe kwa
kibaguzi ikiwemo ile kutoka akaunti ya mtu anayejiita @CraigSainsbury
ambayo ilisomeka: 'F*** you Mario you f****** n*****. Got eat some
bananas and get ebola you dirty monkey.' Hakuna haja ya kutafsiri
kwasababu ya kimaadili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni