Michael Carrick (katikati akiwa na Chris Smalling na Ryan Giggs) anaweza kucheza nafasi ya beki wa kati Manchester United
MAJANGA ya safu ya ulinzi ya Manchester
United yamemfanya kocha Louis van Gaal afikirie kumtumia kwa dharula
Michael Carrick katika nafasi ya beki wa kati.
Carrick ambaye ni kiungo wa kati bado
anasubiri kuanza mechi yake ya kwanza chini ya kocha mpya na anaimarika
pole pole kutoka kwenye majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata majira ya
kiangazi.
Lakini kiungo huyo mwenye miaka 33
ameanza mazoezi uwanja wa Carrington na tayari amefanya mazungumzo na
Van Gaal kuhusu uwezekano wa kucheza nafasi ya beki wa kati.
Tyler Blackett (kushoto) na Smalling wote walikuwepo katika kipigo cha 5-3 dhidi ya Leicester jumapili iliyopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni