STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 20 Novemba 2014

BAADA YA PAZIA LA KUFUZU AFCON 2015 KUFUNGWA JANA, ANGALIA TIMU ZILIZO FANIKIWA KUPENYA.. NIGERIA NJE......

MECHI za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Equatorial Guinea zimefikia tamati jana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefuzu kama mshindi wa tatu bora.
Kongo imekamilisha nafasi ya mwisho katika siti za ndege za kwenda Equatorial Guinea 2015 baada ya kuwa timu iliyomaliza nafasi ya tatu ikiwa na wastani mzuri zaidi wa matokeo kutoka makudi yote saba.
Mabingwa hao wa mwaka 1968 na 1974, walipata nafasi hiyo baada ya Misri kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wao wa Kaskazini mwa Afrika, Tunisia katika Kundi G mjini Monastir.
DRC wamefuzu kama washindi wa tatu wa bora, wakiipiku Misri

DRC ambayo iliifunga Sierra Leone 3-1 mjini Kinshasa, imemaliza na pointi tisa, ambazo ni nyingi zaidi kwa timu zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yote saba.
Mabingwa mara saba, Misri, wameshindwa kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Tunisia kutoka nyuma na kuwafunga. Mafarao, waliongoza hadi mapumziko kwa bao la mshambuliaji wa Chelsea, Mohamed Salah kabla ya Tunisia kuzinduka na kupata mabao kupitia kwa Yassine Chikaoui dakika ya 52 na Whabi Khazri dakika tisa kabla ya filimbi ya mwisho.
Nchi zilizofuzu AFCON ya mwakani mbali ya wenyeji Equatorial Guinea; ni Algeria, Burkina Faso, Cape Verde, Cameroon, Kongo, Ivory Coast, DRC, Gabon, Ghana, Guinea, Mali, Senegal, Afrika Kusini, Tunisia na Zambia.
Saydou Keita ameiongoza Mali kufuzu jana
MSIMAMO WA MAKUNDI BAADA YA MECHI ZA KUFUZU AFCON 2015
Kundi A
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 A. Kusini 6 3 3 0 9 3 6 12
2 Congo 6 3 1 2 6 6 0 10
3 Nigeria 6 2 2 2 9 7 2 8
4 Sudan 6 1 0 5 3 11 -8 3

Kundi B
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Algeria 6 5 0 1 11 4 7 15
2 Mali 6 3 0 3 8 6 2 9
3 Malawi 6 2 1 3 5 9 -4 7
4 Ethiopia 6 1 1 4 7 12 -5 4

Kundi C
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Gabon 6 3 3 0 9 4 5 12
2 Burkina Faso 6 3 2 1 8 4 4 11
3 Angola 6 1 3 2 5 5 0 6
4 Lesotho 6 0 2 4 3 12 -9 2
Group D

Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Cameroon 6 4 2 0 9 1 8 14
2 Ivory Coast 6 3 1 2 13 11 2 10
3 DRC          6 3 0 3 10 9 1 9
4 Sierra Leone 6 0 1 5 3 14 -11 1

Kundi E
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Ghana 6 3 2 1 11 7 4 11
2 Guinea 6 3 1 2 10 8 2 10
3 Uganda 6 2 1 3 4 5 -1 7
4 Togo        6 2 0 4 7 12 -5 6

Kundi F
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Cape Verde  6 4 0 2 9 6 3 12
2 Zambia 6 3 2 1 6 2 4 11
3 Msumbiji  6 1 3 2 4 4 0 6
4 Niger 6 0 3 3 4 11 -7 3

Kundi G
Timu  P W D L GF GA GD Pts
1 Tunisia 6 4 2 0 6 2 4 14
2 Senegal 6 4 1 1 8 1 7 13
3 Misri  6 2 0 4 5 6 -1 6
4 Botswana 6 0 1 5 1 11 -10 1
Ivory Coast imefuzu
pia
Fainali za Mataifa ya Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox