STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 14 Novemba 2014

KOCHA LOUIS VAN GAAL ADOKEZA WANNE KUIKOSA ARSENAL

LOUIS VAN GAAL amedokeza kuwa Wachezaji wake Majeruhi Wanne watashindwa kuwa fiti kuikabili Arsenal.
Majeruhi hao Wanne ni Radamel Falcao, Jonny Evans, Phil Jones na Rafael ambao walidhaniwa watapona mapema kuivaa Arsenal huko Emirates hapo Novemba 22 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Louis van Gaal at the end of the game
Hata hivyo, Van Gaal amekiri kuwa ingawa hawataweza kuanza Mechi na Arsenal lakini upo uwezekano wa Falcao na Rafael kucheza sehemu ya Mechi hiyo.
Amesema "Hapana, sidhani kama wao wataanza kwa sababu baadhi yao wamekuwa nje Wiki tano, sita, saba hivi. Wanaweza kukaa Benchi na kucheza Dakika 20 lakini siwezi kuweka Wachezaji wengi ambao hawako Asilimia 100 Benchi!”
Manchester United's Juan Mata celebrates his goal with teammates Robin van Persie and Wayne Rooney
Kuelekea kwenye Mechi na Arsenal, kulikuwa na dhana kubwa Falcao atakuwa fiti kuivaa Arsenal hasa baada ya kujitangaza mwenyewe mtandaoni kwamba yuko fiti na yupo Mazoezini.
Manchester United Manager Louis van Gaal looks thoughtful at Half time
Majeruhi wa Man United ambao wataikosa Mechi hiyo na Arsenal ni Phil Jones, Jonny Evans na Marcos Rojo lakini Chris Smalling, baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi moja, huenda akaanza kama Sentahafu kushirikiana na Chipukizi Paddy McNair kwenye Difensi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox