STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 14 Novemba 2014

DANIEL STURRIDGE AANZA MAZOEZI

Straika wa Liverpool Daniel Sturridge ameanza tena Mazoezi tangu aumie Musuli za Pajani [Hamstring] Mwezi Agosti akiwa na Timu ya Taifa ya England.
Kukosekana kwa Straika huyo ambae ndie amegeuka mtambo wa Magoli wa Liverpool kumewafanya washinde Mechi 4 tu kati ya 14 ambazo amezikosa.

Sturridge, ambae alifunga Bao 21 katika Mechi 29 za Ligi Msimu uliopita, alikaribia kurejea Uwanjani Mwezi uliopita lakini akapata maumivu mengine Mguuni yaliyomweka nje kwa kipindi kingine.
Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers anategemea Sturridge atakuwa fiti kucheza Mechi yao inayokuja ya Ugenini ya Ligi Kuu England na Crystal Palace hapo Novemba 23.

Msimu huu, Sturridge amecheza Mechi 3 tu za Ligi na kufunga Bao walipocheza Anfield Agosti 17 na kuifunga Southampton 2-1.
Kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, Liverpool wapo Nafasi ya 11 wakiwa Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea na hawajashinda katika Mechi 3 zilizopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox