Beki
wa Everton, Seamus Coleman anahusishwa kusajiliwa na Manchester United
wakati huu wanahitaji kutatua tatizo la beki wa kulia
Manchester
United wanatarajia kuwa na kikao leo ijumaa kuamua kama wanahitaji
kutumia fedha nyingi kuboresha safu ya ulinzi wiki mbili zijazo.
Kocha
wa United, Louis van Gaal anakutana na viongozi wa klabu hiyo kuweka
mipango ya usajili katika dirisha dogo na majira ya kiangazi mwaka huu.
Kununua beki wa kulia itakuwa ajenda kubwa ambapo rada zao zinaangaza kumnasa beki wa Everton mwenye miaka 26, Seamus Coleman au wa Southampton, Nathaniel Clyne mwenye miaka 23.
Beki wa Southampton, Nathaniel Clyne (kushoto) pia anahusishwa kusajiliwa na mashetani wekundu.
Van
Gaal ambaye tayari ameshatumia paundi milioni 156 tangu majira ya
kiangazi mwaka jana, anahitaji kuimarisha kikosi chake kwa lengo la
kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni