Kocha wa
Manchester United, Louis Van Gaal amemtaka mshambuliaji wake raia wa Mexico,
Javier Hernandez 'Chicharito' kufunga mkanda kama anahitaji kudumu kikosini hapo.
Hernandez ambaye
msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid, hivi sasa
amerejea na anatarajiwa kujiunga kambini na wenzake 25 Julai huko nchini Marekani.
Van Gaal
ambaye hakuona nafasi ya Hernandez kikosini hapo msimu uliopita mara baada ya
uwepo wa washambuliaji Radamel Falcao Garcia, Robin Van Persie huku Wayne
Rooney pia akicheza nafasi hiyo.
Van Gaal akiongea
na waandishi wa habari wikiendi hii amethibitisha kumpa nafasi Hernandez,
lakini akasisitiza anatakiwa atumie nafasi hiyo.
Hadi sasa
United wana Rooney, Wilson na Hernandez pekee kama washambuliaji wa kati lakini
Van Gaal yuko relaxed akiamini ni wakati wa Rooney sasa kuongoza jahazi.
Wakati huo
huo klabu ya Manchester United iko mbioni kusaka saini ya golikipa Sergio Romero
wa timu ya taifa ya Argentina aliyepo huru hivi sasa.
Sergio Romero
ambaye amemaliza mkataba na klabu ya Sampdoria anawindwa pia na Real Madrid. United
wanajiandaa kutafuta mbadala wa Victor Valdez ambaye anatimka klabuni hapo
baada ya kukosana na kocha Louis Van Gaal.
Kwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED
JibuFutaKwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED
JibuFutaKwangu ni sawa kupewa nafasi kwa mara nyengine tena kijana wetu #GGMUNITED
JibuFuta