Supastaa wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho 'Gaucho' ametambulishwa
rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki wa klabu ya Fluminense wakielekea
kucheza mechi ya watani wa jadi dhidi ya Vasco Da Gama kwenye uwanja wa
Maracana, Brazil.
Mshindhi
huyo mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA (2004, 2005)
ambaye amesaini klabu hiyo ya Brazil akiwa mchezaji huru, amepokelewa
kishujaa uwanjani na kupewa jezi yake ya heshima, namba 10.
Ronaldinho aliripotiwa kwamba angetua Uturuki majira haya ya kiangazi baada ya kumalizana na klabu ya Queretaro ya Mexixo, lakini kiungo huyo mshambuliaji ameeleza sababu za kurudi Brazil.
"Natamani kuweka historia katika klabu hii." Amesema Ronaldinho wakati wa kutambulishwa.
"Kilichonishawishi
mimi ni kukosa ubingwa wowote wa Brazil. Imenishawishi sana. Hii ni
klabu kubwa yenye wachezaji wakubwa, tuna kila kitu cha kutufanya kuwa
mabingwa"
Ronaldinho
mwenye miaka 35, alianza kucheza mpira katika timu yake ya nyumbani ya
Club Gremio ya Mjini Porto Alegre kabla ya kwenda Ulaya ambako
alizichezea Paris Saint Germain, Barcelona na AC Milan.
Pia alirejea Brazil kuichezea Flamengo na baadaye akaijiunga na Atletico Mineiro ambapo alitwaa kombe la klabu bingwa America Kusini, ' Copa Libertadores' mwaka 2013.
Mashabiki
wa soka Duniani kote wanafurahi kuona fundi mkubwa wa soka kuwahi
kutokea Duniani bado anaendelea kucheza na hana mpango kwa kustaafu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni