ARSENE WENGER amemaliza biashara ya usajili wa dirisha dogo kufuatia kuinasa saini ya Gabriel Paulista.
Dirisha dogo la usajili linafungwa jumatatu ijayo usiku, lakini kufanikiwa kumsajili Gabriel
na Krystian Bielik, Wenger - ambaye amesema kuwa Francis Coquelin ana
asilimia 99 za kusaini mkataba mpya--kitabu chake cha hundi ya usajili
bado kipo wazi.
"Kama
naamka asubuhi na kumkuta mtu amesimama mbele ya mlango wangu ambaye ni
mchezaji mwenye sifa za pekee, nitafungua mlango,".
Wenger alisema:"Bado sijamaliza kabisa. Naweza kutoa anuani yangu kama mnataka"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni