Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia goli lake
MICHUANO ya
Mataifa ya Afrika, Afcon 2015 imeanza kutimua vumbi nchini Guinea ya Ikweta kwa
mechi mbili za kundi A kupigwa siku ya ufunguzi.
Mechi ya kwanza
iliyoanza majira ya saa 1:00 usiku jana, wenyeji Guinea ya Ikweta walilazimisha
sare ya kufungana bao 1-1 na Congo Brazaville.
Guinea ndio
walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Emilio Nsue,
lakini Congo walisawazisha dakika ya 87’ kupitia Thievy Bifouma.
Mechi ya pili
iliyomalizika iliyoanza saa 4:00 usiku, Gabon walipata ushindi wa magoli 2-0
dhidi ya Burkina Faso.
Mabao ya Gabon yalifungwa
na Pierre-Emerick Aubameyang katika dakika ya 19 na Malick Evouna katika dakika
ya 72.
Kwa matokeo hayo,
Gabon wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 3 ambapo wamecheza mechi moja,
wameshinda moja na hawajafungwa.
Nafasi ya pili
inashikwa na Gabon wanaofanana kwa kila kitu na Congo Brazaville katika nafasi
ya tatu.
Wote wamecheza
mechi moja, wametoa sare moja, wamefungana goli moja moja.
Burkina Faso
wanaburuza mkia katika kundi A baada ya kufungwa mechi yao ya kwanza usiku huu.
RATIBA YA MECHI
ZA LEO KUNDI B
Africa Cup of Nations - Group BJanuary 18 | |||
---|---|---|---|
19:00 | ? - ? | ||
22:00 | ? - ? |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni