Wachezaji wa Ghana wakishangilia ushindi wao mbele ya kocha Avram Grant
NDOTO
za Equatorial Guinea kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa,
Afcon 2015 baada ya kufungwa mabao 3-0 na Ghana, lakini aibu kubwa
imetawala baada ya mashabiki wa timu mwenyeji kufanya vurugu kubwa
katika uwanja wa Malabo jana usiku na kusababisha mechi kusimama kwa
dakika 35.
Wenyeji
wameonesha kiwango kikubwa na maajabu makubwa katika michuano ya mwaka
huu, lakini kutolewa hatua ya nusu fainali kuliwaudhi mashabiki ambao
walirusha chupa kwa wachezaji wa Ghana, viongozi na mashabiki.
Wachezaji wakisubiri Helkopta iwatulize mashabiki ili mechi iendelee
Mashabiki wakificha nyuso zao wakati Helkopta inapita juu yao
Polisi wakipiga mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki waliokuwa wanafanya vurugu uwanja wa Malabo
Wachezaji wa Ghana wakitolewa chini ya ulinzi mkali
Shabiki wa Guinea ya Ikweta akiwa ametiwa mbaroni
GHANA IMEISHINDA EQUATORIAL GUINEA NA KUTINGA FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA. LAKINI MECHI HIYO ILITAWALIWA NA TAFRANI ZA KUFA MTU NA HIVI NDIYO HALI ILIVYOKUWA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni