Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amejiuzulu wadhifa wake ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangua akalie kiti hicho.
Tiboroha ameandika barua ya kujiudhuru kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kwa sababu alizoziita za “kujikita zaidi katika kazi yake ya uhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam’.
Habari za ndani ya Yanga zinasema kujiuzulu kwa Tiboroha si jambo la kushtukiza kwani kumekuwa na msuguano kwa muda sasa kati ya pande mbalimbali.
Inadaiwa suala la Niyonzima pamoja na usajili wa wachezaji na kutolewa mlangoni kwa baadhi ya makomandoo kulizua vita ya kimaslahi ndani ya klabu hio.
Habari zaidi zinadai, Tiboroha aliamua kung’atuka baada ya kuwepo taarifa za nafasi yake kupewa mkurugenzi wa fedha, Baraka Deusdith kuikaimu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni