Mzunguko
wa tatu wa michuano wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
unatarajiwa kuendelea wikiendi hii mpaka katikati ya juma lijalo kwa
michezo 13 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Kesho
Jumamosi michezo mitatu itachezwa, mjini Morogoro Burkinfaso FC
watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini humo, Pamba FC
watawakaribisha Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, huku
Ndanda FC wakichea dhidi ya Mshikamno FC katika Uwanja wa Nagwanda
Sijaona Mtwara.
Jumapili
michuano hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, jijini Dar es salaam Young
Africans watawakaribisha Friends Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji
watakua wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Amani Njombe, huku Stand
United wakicheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Michuano
hiyo itaendelea Jumatatu, Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers
katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC dhidi ya
Madini FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi na Africa Lyon wakiwa wenyeji
wa Azam FC uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Jumanne
Mtibwa Sugar watawakaribisha Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Wambi Mafinga, Africa
Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga, na Geita Gold
watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini
Geita.
Singida
United watacheza dhidi ya Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa
Namfua mjini Singida, na mchezo wa mwisho utachezwa Februari Mosi katika
ya Wenda FC dhidi ya Mbeya City uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mpaka
sasa timu ya JKT Mlale pekee ndio imeshafuzu kwa mzunguko wa nne baada
ya kuiondosha Majimaji kwa mabao 2-1, katia mchezo uliochezwa wiki
iliyopita kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni