Refa Seechurn Rajindraparsad |
Polisi wakimlinda mwamuzi Rajindraparsad asipewe kichapo na wachezaji wa Tunisia baada ya kutoa penati tata kwa wenyeji dakika za lala salama |
Mwamuzi huyo kutoka Mauritius alitoa penati ya utata dakika za lala salama za pambano hilo na kuwapa wenyeji bao la kusawazisha lililofanya mchezo huo kuongezewa muda wa dakika 30 na Guinea ya Ikweta kushinda kwa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali.
Wachezaji wa Tunisia walionyeshwa kukerwa na maamuzi hayo kias cha askari Polisi kulazimika kumuokoa na kumlinda ili asidhiriwe.
Katika taarifa yake iliyotolewa juzi, CAF imetangaza kuondoa mwamuzi huyo kwa kuchezesha ovyo mechi hiyo na msimamisha kwa muda wa miezi sita sambamba na kumuondoa kwenye orodha ya Caf ya waamuzi wa Daraja A kutokana na kikao cha Kamati ya waamuzi.
Mwamuzi huyo licha ya 'kubanyanga' mchezo huo ambao ulionekana wazi wenyeji wameondoshwa mashindanoni, alilitaka shirikisho la TFT kumuomba radhi kwa vitendo alivyofanyiwa na wachezaji wa Tunisia siku ya mchezo huo.
"kwa ku utokana na ukweli mchezaji wa Guinea ya Ikweta alionekana kujirusha baada ya kuguswa
Tunisia dhidi ya wenyeji Guinea ya Ikweta aliyedaiwa kuwabeba wenyeji kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Tunisia na kumtaka kuliomba radhi Shirikisho la Soka la Tunisia kwa kilichotokea.
TFT tayari imeshaadhibiwa kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wa timu yao ya taifa na maafisa wake, ingawa CAF kupitia kamati ya Waamuzi inakiri kwamba mwamuzi wa pambano hilo alivurunda kwa kucheza chini ya kiwango jambo ambalo CAF haipo tayari kuona madudu kama hayo katika michuano yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni