Kipigo cha mabao 3-0 ugenini
dhidi ya El-Merrikh ya Sudan, kimemponza kocha Joseph Omog baada ya
uongozi wa Azam FC kuamua kumtimua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa Azam FC
muda mfupi uliopita, Uongozi wa Azam FC umetangaza kumtimua raia huyo wa
Cameroon.
Taarifa hiyo inasomeka: "Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni