Sare ya bao 2-2 ndiyo iliyoing'oa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Luiz akiwa kati ya wafungaji.
Luiz amefunga bao la kwanza la kusawazisha na
kuisaidia PSG kuing’oa Chelsea. Awali alitangaza hatashangilia akiwa Stamford
Bridge katika mechi hiyo ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa, lakini alishindwa
kujizuia baada ya kufunga bao safi la kichwa.
Awali mashabiki walikuwa wakimsomea kila alipokamata mpira na dakika chache baadaye akafunga bao hilo.
Luiz alijiunga na PSG kwa kitita cha pauni
milioni 50 akitokea Chelsea.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, beki
huyo amewaambia mashabiki wa Chelsea wamuwie radhi kwa kuwa alikuwa akipambana
kwa ajili ya kazi yake na hakulenga kuwaumiza miezi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni