Kocha
wa zamani wa klabu ya Manchester City ambae kwa sasa anainoa Intermilan
Roberto Mancini amesema anaamini kuwa kiungo mchezeshaji wa klabu ya
manchester city Raia wa Ivory Coast Yaya Toure atajiunga na miamba hao
wa soka wa Nchini Italia baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia ya
kuondoka katika dimba la Etihad msimu ujao.
Yaya
ambaye amekuwa na kiwango kibovu tangu aipe timu yake ya Ivory Coast
ushindi na kutwaa kombe la Mataifa Barani Afrika sasa huenda njia yake
ikawa nyeupe kutoka Manchester City, baada ya kutua kwa viungo kama vile
Fernando pamoja na Fernandinho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni