Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, nchini Tanzania, Hussein Machozi, amefunguka kuwa huenda mwakani (2016) akasajiliwa na timu ya Kagera Sugar, na hivyo kuwataka mashabiki wake kutoshangaa katika hilo.
Akihojiwa amesema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi makali ya kuweza kufuzu vigezo vya kuwa mmoja wa wanasoka wa timu hiyo katika msimu wa ligi kuu Tanzania Bara mwakani.
Amesema kuwa amekuwa akitembelewa kila siku na watu wa Kagera Sugar, hivyo nguvu nyingi amezielekeza huko ili kuweza kung’ara na timu hiyo msimu ujao na kuwataka mashabiki kukaa mkao wa kula katika soka.
Ikumbuke kuwa kabla ya kuanza muziki mwanamuiki huyo alikuwa msakata kabumbu mzuri na kwa uamuzi huo ni sawa na kurudi tena uwanja wa nyumbani ingawa hajatoa tamko kama anaachana na muziki au la.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni