STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 13 Mei 2015

KWA TAARIFA YAKO: UCHAMBUZI KUHUSU GEMU YA LEO




Jana tumeshuhudia wana wa Catalunya wakitimba hatua ya fainal zitakazo fanyika pale Ujerumani ktk jiji la Berlin mnamo tarehe 6/6/2015. 

Hii leo viunga vya jiji la Kifalme ktk dimba la Santiago Bernabeu Real Madrid wata wakabili wana wa Torino kibibi kizee Juventus. Mchezo wa awamu ya kwanza Real walipoteza 2-1 magoli ya Juve yalifungwa na Morata pamoja na Tevez huku C.ronaldo aki ifungia Real. 

 Kwa ujumla timu hizi zimekutana mara 17 na kila timu iki ibuka na ushindi mara 8 tukishuhudia sare moja ya msimu wa 2013/14. Vercchia Signora ama kwa lugha nyepesi waite kibibi kizee wanaoneka kuwa bora zaidi ktk mtoano mbele ya Los Blancos mara nne walizo kutana wameshinda mara tatu dhidi ya moja walio poteza kwenye fainal ya mwaka 1998 pale Amsterdam Arena goli la Real likifungwa na Predrag Mijatoviç dakika ya 66 Juve enzi hizo ikiwa chini ya Marcelo Lippi na Real chini ya Jupp Heynckes ktk ubingwa wao wa 7 baada ya miaka 23.

 Vijana wa Carlo Ancelotti wanajivunia kuwa na historia nzuri ktk dimba lao la nyumbani mbele ya Juve kwani wameshinda mara nne kati ya tano. Uzuri wa timu hizi pindi zikikutana lazima mbabe ajulikane hususani hatua ya mtoano msimu wa 1995/96 Juve waliwatoa Real kwa jumla ya magoli 2-1 na kwenda kuchukua ubingwa wao wa pili na wa mwisho kwenye michuano hii kwa kuwashinda Ajax kwenye mikwaju ya penalti pale Stadio Olimpico Roma.

 2002-03 Kibibi kizee baada ya kupoteza 98 wakawatoa Real kwa jumla ya magoli 4-3 kabla ya kwenda kupoteza kwa mikwaju ya penalti mbele ya Ac Milan. Msimu wa 2004/05 Real wakapoteza hatua ya 16 bora kwa Juve wakitoka kwa jumla ya magoli 2-1.

 Ndani ya Bernabeu Real wamepoteza michezo 6 dhidi ya timu za Uitaliano na kushinda michezo 21 kati ya 29 iliyochezwa. Kumbuka kwenye mchezo huu kuna spidi 120 nikimanisha idadi ya vikombe kwa timu hizi ktk michuano mbalimbali Real wakiwa na 70 Juventus 50.

 Si hivyo tu kwani tunapata vikombe vya Uefa 12 kwenye mtanange huu Madrid wakiwa navyo 10 kibibi kizee kikijikongoja na 2.
 Usisahau namba 20 ina simama kama mjumuisho wa timu hizi kucheza fainal za Uefa Blancos mara 13 Vecchia Signora Juve fainal 7.

 Mpaka sasa C. Ronaldo ana goli 9 Tevez upande wa Juve ana goli 7, pia Ronaldo anaongoza orodha ya wachezaji walio piga mashuti mengi kulenga lango 29 wakati Tevez akishika nafasi ya 3 kwa mashuti 17. 

Kwa kuangazia mtanange wenyewe kikosi cha Massimiliano Allegri kitachagizwa na urejeo wa Pogba wakati Ancelloti akiwa ana haha na hatma ya Kroos achilia mbali vuguvugu la wakala wa Bale kuhusu mchezaji huyo kutengwa uwanjani na wenzake. 

 Shughuli pevu itakuwa ni safu ya kiungo kwa timu hizi na pengine tutaraji mashambulizi ya kustukiza kwa pande zote si taraji Juve kupaki basi kwani itawaweka kwenye wakati mgumu sana kutokana na Real kutafuta goli moja tu pasipo wa kuruhusu kufungwa. 

 Mipira ya adhabu inaweza kuamua matokeo kwa pande zote pande zote ili kupata matokeo ni kucheza mchezo wa spidi na kuepuka faulo ktk maeneo hatarishi na uki uwangazia mchezo huu kwa undani huenda tukashuhudia sare.
 Sina mengi sana ktk mchezo huu cha msingi tusubiri mwamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson kupuliza kipenga kisha tujue fainal ni El Classico au ni Blaugrana dhidi ya Vecchia Signora. 


 For more/ Ushauri:: Choikangta.ckt@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox