Ndemla (kulia) akisaini mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva (kushoto)
WEKUNDU
wa Msimbazi, Simba wameanza harakati za kuwabakisha nyota wake
waliomaliza mikataba baada ya jioni ya leo kumsainisha mkataba wa miaka
mitatu (3) kiungo wake mchezeshaji, Said Ndemla.
Ndemla
amesaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva wenye thamani
ya shilingi milioni 40 za Kitanzania jumlisha gari aina ya IST.
Nyota huyo zao la Simba B atakuwa analipwa mshahara wa milioni mbili (2) kwa mwezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni