MCHEZO wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Kundi A
Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Medeama FC ya Ghana
utaonyeshwa moja kwa moja na Azam TV.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi, unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga nchini kote na kurushwa moja kwa moja na Azam TV ni faraja kwa wapenzi wa timu hiyo waishio nje ya Jiji hilo.
Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani,
Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa
na mchezo wa tatu wa kundi lake, wakati Medeama inatarajiwa kuwasili kuanzia
leo.
Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni