Mkataba mpya wa Azam Media kurusha matangazo Live ya Ligi Kuu Bara utagharimu Sh bilioni 23.
Mkataba wa awali, kila klabu ilikuwa inapata Sh milioni 100 kwa msimu lakini sasa itaingiza karibu mara mbili ya hizo.
Katika mkataba uliosainiwa leo, klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126.
Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi.
Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.
Maana
yake ligi itakapoisha, zitazokuwa juu kimsimamo zitapata fedha nyingi
zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu.
Lengo
kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu
wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali itakayochangia ushindani
uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili mwisho wa
ligi ifaidike.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni