klabu ya TP Mazembe imehitimisha ushiriki wa Yanga katika mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya Nane kwa kipigo cha mabao 3-1 leo jioni.
Katika pambano hilo la kukamilisha ratiba kwa Yanga, kikosi cha TP Mazembe kilipata mabao yake kupitia kwa Jonathan Bolingi dakika ya 28, Rainford Kalaba dakika ya 54 na 64.
Amissi Tambwe aliifungia Yanga bao la kufutia machozi dakika ya 75
Katika mchezo wa leo, Yanga ilicheza pungufu tangu dakika ya 30, baada ya beki wake chipukizi, Andrew Vincent Chikupe ‘Dante’ kutolewa kwa kadi nyekundu.
Beki huyo aliyesajiliwa Mei mwaka huu kutoka Mtibwa Sugar alitolewa dakika mbili tu baada ya Mazembe kupata bao la kwanza lililofungwa na Jonathan Bolingi, aliyemalizia pasi ya Deo Kanda.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke/Matheo Anthony dk86, Said Juma ‘Makapu’/Oscar Joshua dk78, Amissi Tambwe na Simon Msuva/Juma Mahadhi dk68.
TP Mazembe; Sylvain Gbohouo, Jean Kasusula, Joel Kimwaki, Djo Issama, Chirstian Luyindama, Solomon Asante, Christian Koffi, Daniel Adjei Nii, Ranford Kalaba/ Yaw Frimpong dk84, Deo Kanda/Adama Traore dk71 na Jonathan Bolingi/ Chavda Maisha dk74.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni