Usiku wa August 25 nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ambaye anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji, jina lake lilirudi tena kwenye headlines kufuatia ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Lokomotiva Zagreb walioupata wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminas Arena.
Katika ushindi huo wa goli 2-0 walioupata KRC Genk katika michuano ya kuwania kucheza hatua ya Makundi ya Europa League unawawezesha kufuzu hatua hiyo moja kwa moja kutokana na mchezo wao wa kwanza dhidi ya Lokomotiva walitoka sare ya goli 2-2.
Samatta anaiwezesha Genk kufuzu hatua ya makundi kwa mafanikio kutokana na kufunga goli la kwanza dakika ya 2 na baadae mjamaica Leon Bailey akafunga goli la pili, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Samatta kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Europa League.
STORI YA PILI;
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo usiku wa August 25 aliingia katika historia mpya ya soka lake, hiyo inatokana na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya wa mwaka kwa kuwashinda wapinzani wake Antoine Griezmann wa Atletico Madridi na timu ya taifa ya Ufaransa, pamoja na Gareth Bale.
Ronaldo anafanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kumaliza msimu wa 2015/2016 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuiwezesha Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na kufikisha rekodi ya kutwaa Kombe hilo mara tatu katika historia yake ya soka.
Hata hivyo msimu wa 2015/2016 licha ya kuiwezesha Ureno kutwaa taji la Euro 2016 kwa mara ya kwanza katika historia, Ronaldo akiwa na Real Madrid msimu wa 2015/2016 alikuwa kafunga jumla ya goli 51 katika mechi zake 48 alizocheza pamoja na kutoa assist 15, lakini akiwa na rekodi ya kufunga magoli 16 katika mechi 12 za UEFA Champions league.
STORI YA TATU;
Ratiba
kamaili ya hatua ya makundi ya Uefa champions League imetoka.
Timu za
Uingereza zinaonekana kuwa na ahueni kwenye hatua hii kutokana na
kutokuwa kwenye makundi ya vifo huku Leicester wakiwa kwenye kundi
ambalo unaweza kuliita jepesi zaidi.
Kwa
ratiba hii unatakiwa kuwa na matarajio ya kushuhudia moja ya hatua 16
bora nzuri na yenye ushindani zaidi kwa uwezekano wa vilabu vikubwa
kubaki kwenye hatua ya makundi ni mdogo sana.
Group A fixtures
Group C fixtures
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni