Jumatano hakutakuwa na mchezo wowote wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kutokana na wachezaji wa Yanga SC kwenda katika timu za Taifa.
Mabingwa watetezi wa VPL wachezaji wake 9 watakuwa katika majukumu na timu zao za Taifa hivyo wamelazimika kuvunja kambi jana na wataingia kambini Jumatatu Ijayo ili kujiandaaa na mechi yao na Ndanda ya Mtwara itakayochezwa Mtwara siku ya Jumatano Septemba 7,hivyo mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliotakiwa kupigwa Agosti 31 unaendelea kuwa kiporo.
Katika orodha hiyo ya wachezaji 9, wanandinga 6 wa Yanga wanajiunga na Timu ya Taifa ya kandanda ya Tanzania, Taifa Stars, ambao ni Deogratius Munishi ,Kelvin Yondani ,Vicent Andrew ,Mwinyi Haji ,Juma Mahadhi na Simon Msuva
Kwa upande wa kimataifa, Tayari Vicent Bossou imeripotiwa kusafiri jana usiku kuelekea kwao Togo kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Wengine ni Haruna Niyonzima anayekwenda kujiunga na Timu ya Taifa ya soka ya Rwanda, Amavubi, huku Amissi Tambwe akielekea kujiunga na timu ya Taifa ya Burundi, Intamba Murugamba.
STORI YA PILI;
Chelsea wameanza vizuri mbio za kuwania ubingwa wa EPL chini ya kocha wao mpya Antonio Conte.
Wameshinda mechi zote tatu na kujikusanyia alama 9 kibindoni sambamba na Manchester City na Man United.
Lakini pamoja na yote hayo mambo si shwari kwa kiungo Cesc Fabregas ambaye ni bingwa wa kutoa pasi za mwisho.
Ujio wa N’Golo Kante ndiyo sababu kubwa ya Cesc Fabregas kukosa nafasi yake kwenye kikosi hicho kilicho chini ya Muitaliano Antonio Conte.
Hali hii imezua tetesi kwamba Muhispaniola juyo yuko mbioni kuondoka klabuni hapo huku gazeti la El Confidencial likiripoti kuwa kocha wake Conte amemuwashia taa ya kijana kuondoka klabuni hapo.
Cesc afunguka kwenye ukurasa wake wa Instagram
Baada ta tetesi hizo kuzidi mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona ameandika haya kwenye Instagram yake.
"Contrary to what has been written, the manager and I have a good relationship and he has NEVER told me that I can leave. He said that he counts on me, as I count on him. I will continue to fight for this club until the very end and when called upon I will always give my very best. I'm fully committed to @chelseafc and my only goal is to help them win more trophies. #ChelseaFC."
"Kinyume na ambavyo imekuwa ikiandikwa, uhusiano wangu na meneja ni mzuri na kamwe hajawahi kuniambia kwamba naweza kuondoka klabuni. Alichokisema ni kwamba bado ananihesabia, kama ambavyo mimi namhesabia pia. Nitaendelea kupambana kwa kila hali mpaka mwisho, na meneja atakaponipa nafasi nitapambana kwa juhudi zangu zote. Bado nina moyo ule ule wa kujitolea klabuni hapa@chelseafc na lengo langu kuu ni kuhakikisha naisaidia timu kushinda mataji mengi zaidi. #ChelseaFC"
STORI YA TATU;
Sergio Aguero anaweza kufungiwa michezo mitatu baada ya kumpika kiwiko beki wa West Ham Winston Reid jana na kuwa na uwezekano wa kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United.
Mshambulizi huyo alimfanyia tukio hilo Reid kuelekea mwishoni mwa mchezo huo ambao City walishinda 3-1, mabao yaliyofungwa na Raheem Sterling (2) na Ferndandinho. Reid alitolewa mara moja baada ya tukio hilo na kocha wake Slaven Bilic amsema alifanya hivyo kutokana na sababu za kiufundi.
Mwamuzi wa mchezo huo Andre Marriner alikuwa karibu kabisa wakati tukio lile likitokea. Aliamuru ipigwe free-kick na imeonekana kwamba hakujua kama Aguero alifanya kitendo kile. Lakini pamoja na yote hayo FA wanaweza kuangalia upya video na kuitolea maamuzi.
Endapo Aguero atakumbana na adhabu hiyo, basi anaweza kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United utakaopigwa Old Trafford Septemba 10, mchezo mwingine ukiwa dhidi ya Bournemouth kabla ya kumalizia na Swansea kwenye Kombe la EFL.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni