MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Alexis Sanchez amefanikiwa kutwaa tuzo ya mashabiki ya mchezaji bora wa PFA msimu wa 2014/2015.
Sanchez amepata mafanikio hayo katika msimu wake wa kwanza ikimshinda winga wa Chelsea, Eden Hazard.
Nyota huyo raia wa Chile amefanikiwa kuifungia Arsenal magoli 16 na kutoa pasi za mwisho nane katika mechi za ligi kuu England.
Sanchez ambaye ni miongoni mwa wachezaji 10 waliotajwa kuwania tuzo hiyo na amepata jumla ya kura laki mbili (200,000) akiwapiku Hazard na mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni