MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan amesaini Mkataba wa miaka miwili na Shanghai SIPG na anatarajiwa kutambulishwa katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya China wiki ijayo.
Nahodha huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 29 amesema leo katika tovuti yake kwamba amesaini Mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya ambao kipengele cha kuongezwa..
Vipengele vya Mkataba havijawekwa wazi, lakini inaelezwa mpachika mabao huyo atakuwa analipwa dola za Kimarekani 250,000 kwa wiki ambazo alikuwa analipwa na mabingwa wa UAE, Al Ain.
Taarifa kwenye tovuti ya Gyan imesema mchezaji huyo atatambuliwa Shanghai itakaoorejea kwenye mchezo wa Ligi Kuu na Guangzhou R&F Jumapili.
Gyan aling'ara sana na Al Ain, aliyoichezea kwa miaka minne akifunga mabao 95 katika mechi 83, lakini timu hiyo ya Uarabuni imesema ofa ya timu ya China ilikuwa kubwa kuihimili kumzua mchezaji kuondoka.
Gyan sasa anakuwa mchezaji ghali zaidi China, ambako klabu kubwa zimemwaga fedha kusajili wachezaji waliowika Ulaya kama Demba Ba na Paulinho, huku Mbrazil Robinho akitarajiwa kufuatia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni