Rais wa Fifa, Sep Blatter aliyetangaza kujiuzulu mrithi wake atapatika February |
SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.
Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Sepp Blatter aliyejiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika kupata mrithi wake.
Wakati huo, kundi la watu wanaoshinikiza kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini humo wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza mapinduzi hayo.
Kundi hilo limesema Annan ni mtu makini ambaye anapaswa kuongoza tume ya mageuzi wakati huu Dunia ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.
Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni