Baada ya siku chache zilizopita kutajwa majina ya Wanasoka wanaowania tuzo ya Mchezaji bora Ulaya, tutazame baadhi ya kauli za Wanasoka juu ya miongoni mwa anayepewa kipaumbele cha kutwaa tuzo hii, Lionel Messi.
Arsene Wenger {Kocha, Arsenal} - "Ni nani Mchezaji bora wa dunia? LeoMessi. Ni nani Mchezaji bora ambaye hajawahi kutokea? Leo Messi"
Diego Maradona {Mchezaji na Kocha wa zamani wa Argentina} - "Hatimaye nimemuona Mchezaji ambaye atarithi nafasi yangu kwenye nchi ya Argentina na jina lake ni Messi. Messi ana kipaji na anaweza kuwa Mchezaji bora"
Pele {Mchezaji wa zamani wa Brazil} - "Kwa kipindi hiki, Messi ni bora"
Eidur Gudjohnsen {Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Barcelona} - "Control ya Messi ni bora zaidi sijapata kuona. Kiukweli amejaliwa pumzi"
Rafael van der Vaart {Mchezaji wa zamani wa Tottenham} - "Mchezaji bora wa kuwahi kukutana nae? nazani ni Messi. Alitumaliza kabisa"
Klaas jan Huntelaar {Schalke 04} - "Ni nani zaidi, Messi au Cristiano Ronaldo? Messi. Ronaldo ni bora, lakini Messi ni mara kumi zaidi yake"
Sergio Aguero {Mchezaji wa Man City} - "Messi kawa mchezaji bora mara kibao na bado anaendelea kuwania, atakuwa mchezaji bora mpaka astaafu soka"
Antonio Cassano {Mchezaji wa zamani wa Ac Milan} - "Messi ni Mchezaji bora kabisa katika historia ya soka, ndio maana naipenda Barcelona zaidi ya Real Madrid"
Diego Simione {Kocha, Atletico de Madrid} - "Messi peke yake ni hatari zaidi ya Ronaldo, Bale na Benzema kwa pamoja"
Arda Turan {Atletco, Uturuki} - "Messi au Ronaldo mchezaji bora wa dunia? nitasema Ronaldo. Messi ni kutoka sayari nyingine"
Roy Keane {Mchezaji wa zamani wa Man U} - "Wakati nakua nilikuwa shabiki wa Maradona na kwasasa ni shabiki wa zao lake Ronaldo ila Messi ni zaidi sijapatkuona. Najaribu kutafuta mapungufu yake uwanjani lakini nashindwa"
Bacary Sagna {Mchezaji wa Man City} - "Mchezaji bora niliowahi kukutana naye? Messi, akiwa anacheza katika ubora wake. Ni mchezaji bora wa dunia. Soka linaonekana jepesi sana wakati anacheza"
Javier Mascherano {Barcelona} - "Inawezekana sio binadamu, ni vizuri Messi anajitambua yeye ni nani. Messi anacheza zaidi ya kucheza"
Fabio Capello {Kocha wa zamani wa Juventus} - "Katika maisha yangu sijawahi kumuona mchezaji mwenye kiwango, mwonekano na umri ule mdogo, kwakweli anavaa jezi nzito katika moja ya timu kubwa duniani"
Marcello Lippi {Kocha wa zamani wa Italy} - "Bora??? Messi"
Arjen Robben {Bayen Munich} - "Messi ni mchezaji wa sayari nyingine"
Sir Alex Ferguson {Aliyekuwa Kocha wa Man U} - "Wakosoaji siku zote wanauliza wachezaji wa zamani kama Pele wangeweza kucheza mpira wa kileo. Lionelessi angeweza kucheza miaka ya 50 na sasa kama ambavyo wangefanya Di Stefano, Pele, Maradona, Cruyff kwa sababu wote ni
wachezaji wakubwa. Bila ubishi Messi anafiti kote"
Naamini kuna kitu kipya umekipata Kwenye hizo kauli za wanasoka hao, ila tambua zipo kauli kibao kutoka Kwenye vinywa vya wanasoka wengine wengi kuhusu mshambuliaji huyo hatari aliyeshindwa kufurukuta mara kibao na timu yake ya taifa hali inayompelekea hadi sasa kushindwa
kunyanyua kombe lolote na timu yake ya taifa ya Argentina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni