Kocha wa Simba, Dylan Kerr ameonyesha yeye ni ‘mgumu’ baada ya kusaidiana na ‘masela’ wa mtaani Lushoto na kusukuma gari aina ya Toyota Hiace ambalo lilikuwa na tatizo la kuwaka kwa stati.
Kerr raia wa Uingereza alisukuma gari hilo wakati akitafuta sehemu yenye runinga kwa ajili ya kuangalia fainali ya michuano ya Tenisi ya Wilbeldon kati ya Mmarekani Serna Williams dhidi ya Mhisoania Garbine Muguruza.
Serena alishinda mechi hiyo kwa ulaiini, lakini Kerr alipambana na kuhakikisha anaishuhudia.
Simba ipo kambini Lushoto kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni