Kwa muiibu wa chombo cha habari cha Ujerumani cha Sport1, Manchester United wanajiandaa kutuma ofa mpya kumsajili nyota wa Bayern, Thomas Muller.
Awali
 Man United waliweka mezani ofa ya Euro milioni 82 kuinasa saini ya 
mshindi huyo wa kombe la Dunia 2014, lakini Miamba ya Bavarian ilikataa.
Wakiwa tayari wamemsajili Gwiji wa Bayern, 
Bastian Schweinsteiger,  Louis van Gaal anajiamini kwamba anaweza kumsajili Muller.
Sport1 wanadai kwamba United wapo tayari kulipa Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 69 kumsajili Muller.
Dau hilo limeandaliwa na bosi mwenyewe Ed Woodward.
Kama
 United watamsajili kwa dau hilo, utakuwa usajili ghali zaidi kuwahi 
kufanyika na klabu hiyo wakivunja rekodi ya kumnasa Angel Di Maria kwa 
paundi milioni 59.7 majira ya kiangazi mwaka jana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge 
amewaondoa hofu mashabiki kwamba hakuna mchezaji atakayeuzwa kwa sasa.
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni